global
Site Admin
Topic Author
Posts: 66
Joined: Fri Jul 14, 2017 1:50 pm
Contact:

Vitu muhimu vinavyofanya injini ya Dizeli iwake

Tue Nov 21, 2017 10:16 am

Kwa injini zote zinazowaka kwa ndani yafuatayo lazima yawepo:-
1. Mafuta na hewa lazima yawepo na kwa kipimo kinachohi-tajika.
2. Mafuta na hewa lazima vikandamizwe kabla au baada ya mchanganyiko kutokea.
3. Mchanganyiko unaokandamizwa lazima uwake na utanuke ili uweze kuendesha injini.
4. Moshi wa mchanganyiko uliokwishawaka lazima utoke ndani ya injini ili uache nafasi kwa ajili ya mchanga-nyiko mpya. Nia mbili zitumikazo katika injini zinazowaka kwa ndani huitwa:-
i. Injini zenye mipigo minne ya kurudia.
ii. Injini zenye mipigo miwili
Kwa injini za aina ya kwanza mipigo hiyo ni kama ifuatavyo:-
i. Mpigo wa kuingiza hewa
ii. Mpigo wa mkandamizo. (Compression stroke)
iii. Mpigo wa mnyumbulizo (Ignition stroke)
iv. Mpigo wa kutoa uchafu (Exhaust stroke)
Kwa injini za mipigo miwili, mipigo hiyo ni:-
i. Mpigo wa kuingiza hewa (Induction stroke)
ii. Mpigo wa mnyumbulizo (Ignition stroke)
Mifano mizuri ya injini za mipigo minne ni:-
Injini za gari ndogo au kubwa ziwe za petroli au dizeli.
Injini za ndani kwa kuendesha maboti au meli nazo ni za dizeli.
Kwa injini za mipigo miwili mifano ni:- Injini za nje (Outboard Engine) baadhi ya pikipiki, hizi zinatumia petroli. Injini za ndani (Inboard engine) kuendeshea meli kubwa na zinatumia dizeli.
Kama ilivyo katika nadharia ya injini, tunasema kwamba injini ni mkusanyiko wa vifaa mbali mbali vikubwa na vidogo. Kuna injini zilizo na silinda moja au zaidi ya moja hayo yote hutegemea matakwa ya mtengenezaji, lakini kimsingi maumbile ya injini hayatofautiani sana. Vifaa ambavyo kila injini huwa navyo ni kama ifuatavyo:-
(i) Silinda Bloki
Hiki ni kifaa kikubwa ambamo injini inaungwa na kimetenge-nezwa kamilifu kuweza kuhimili kazi zote za injini. (Angalia picha).
Image
Taswira

(ii) Pisitoni
Kazi yake ni kudhibiti hewa au mchanganyiko wa hewa na mafuta ndani ya silinda. Pia kutoa nguvu itokahayo na kuungua kwa mafuta kupitia mkono wa conekitingi rodi hadi kwenye krankishafuti. (Angalia picha).
Image
Taswira

(iii) Konekitingi Rodi
Huu ni mkono unao unganisha pisitoni kwenye krankishafuti.
Pia unasaidia kusukuma pisitoni chini na juu.
Image
Taswira

(iv) Krankishafuti
Imetengenezwa madhubuti kwa madini maalumu ili kuzuia kupinda wakati injini inapofanya kazi. Kazi yake ni kubadilisha mwendo wa kawaida wa pisitoni ambao ni chini juu kuwa mwendo wa mzunguko.
Image
Taswira

(v) Flaiwili
Hii ni namna ya gurudumu nzito la chuma ambalo hufungwa upande mmoja wa krankishafuti. Kazi yake ni kuisaidia injini iweze kuzunguka vizuri.
Image
Taswira

(vi) Silinda Hedi
Hii ni mfuniko wa silinda. Kazi yake ni kuzuia hewa au hewa na mafuta visitoke nje wakati wa mkandamizo.
Image
Taswira

(vii) Valvu
Valvu ni vizibo vya milango ya hewa au hewa na mafuta inayoingia na kutoka kwenye silinda na chumba cha kuchomea. Kwa kawaida kun aina mbili za valvu, mmoja kwa kuingilia hewa safi, na wapili kutolea hewa chafu.
Image
Taswira

(viii) Kamshaft
Imetengenezwa kwa madini inayovumilia msuguano. Katika mashine kifaa hiki kinaendeshwa na krankishafuti na kazi yake ni kufungua valvu ili kuingiza au kutoa hewa chafu, pia kuendesha vifaa vingine kama pampu za dizeli na pampu ya oili.
Image
Taswira

Vifaa hivi vikubwa na vingine vingi vidogo vidogo ndivyo vinavyo fanya injini iwe na umbo lililo kusudiwa. (Angalia picha).
Image
Taswira

Trending Topics