global
Site Admin
Topic Author
Posts: 66
Joined: Fri Jul 14, 2017 1:50 pm
Contact:

UHAKIKI WA RIWAYA: TAKADINI

Tue Nov 21, 2017 10:38 am

UHAKIKI WA RIWAYA: TAKADINI

MWANDISHI: BEN J. HANSON
WACHAPISHAJI: MATHEWS BOOKSTORE AND STATIONARIES
MWAKA: 2004
MHAKIKI: DAUD MAKOBA 0754 89 53 21/ 0653 25 05 66

TAKADINI ni riwaya inayopaza sauti kuwatetea watu wenye ulemavu. Katika jamii za Kiafrika walemavu hawakupewa kipaumbele. Wengi waliuawa na waliopona walitengwa!

Katika riwaya hii, mwanamke shujaa, Sekai anaukataa ujinga wa jamii yake dhidi ya walemavu. Anajitolea kufa na kupona kutetea uhai wa mwanaye mwenye ulemavu wa ngozi – TAKADINI.

MAUDHUI

DHAMIRA
i.    Ukombozi wa kiutamaduni. Jamii inawatenga watu wenye ulemavu. Mzee Makwati na washikilia mila za kale wengine wanadhamiria kumuua Takadani kwa sababu alizaliwa akiwa mlemavu wa ngozi. Sekai anatoroka na mwanaye ili kumuepusha na balaa hilo.
ii.    Mapenzi. Haya yamejadiliwa katika pande mbili.
-    Upande wa kwanza unazungumzia mapenzi ya kweli. Haya yanaonekana kwa Sekai ambaye anampenda sana mwanaye. Hakuwa tayari kuona mtu yeyote akimdhuru mtoto huyo aliyezaliwa na ulemavu wa ngozi.
-    Pia pasipo kujali ulemavu aliokuwa nao Takadini, msichana Shingai alikubali kuolewa naye hata akamzalia mtoto.
-    Upande wa pili unazungumzia mapenzi yasiyo ya kweli. Mzee Makwati hana mapenzi ya kweli kwa mwanaye Takadini. Yuko tayari kumuangamiza mwanaye ili kutimiza mila za jamii ambazo hata hivyo zimepitwa na wakati.
iii.    Ujasiri. Sekai ni mwanamke jasiri, hakusita kupambana vilivyo ili kumuokoa mwanaye. Ujasiri huu unamfanya atorokee jamii ya mzee Chivero.
iv.    Haki za walemavu. Walemavu wana haki ya kuishi kama watu wengine. Si kweli kuwa kuishi na walemavu kunaweza kusababisha maafa katika jamii. Takadini aliyedhaniwa kuwa angesababisha maafa, anageuka msaada mkubwa katika jamii yake.
v.    Nafasi ya mwanamke katika jamii
-    Jasiri na asiyeogopa chochote. Sekai ni jasiri, anatoroka na mwanaye na kwenda kuishi naye uhamishoni.
-    Mwenye mapenzi ya kweli. Sekai anampenda Takadini, vivyo hivyo, msichana Shingani anampenda kijana huyo bila kujali ulemavu wake wa ngozi na mguu.
-    Asiyekubaliana na mila potofu. Sekai anakataa mila potofu zilizolazimisha kukatisha uhai wa watoto waliozaliwa na ulemavu.
-    Mchapakazi. Sekai anajituma kufanya kazi kwa bidii. Hii inamsaidia mwanaye Takadini kukua vyema

WASILIANA NAMI KWA 0754 89 53 21/ 0653 25 05 66

Trending Topics